| BACK TO LIST | |||
|
(a) Madda kwa sababu ya kutokea hamza; imegawika sehemu tatu:
1. Madda iliyokuwa wajib kuivuta iliyopo kwenye neno moja الْمَدُّ الْواجِبُ الْمُتَّصِلُ
Ikitokezea herufi ya hamza baada ya herufi ya madda katika neno moja, hukmu ya madda hiyo ni kuwajibika kuivuta harakah nne au tano katika hali ya wasl (ya kupita) na harakah sita katika hali ya waqf (ya kusimama). Na inakatazwa kufupisha zaidi ya harakah nne.
Mfano : وَالسَّمَاءِ ، سُوْءُ ، وَجِيْءَ
wassamaAAAAAi, suUUUUUu, wajiIIIIIa
2-Madda inayojuzu kuvutwa au kufupishwa baina ya maneno mawili المد الجاﺌز المنفصل
Neno likimalizikia na herufi ya madda, ikisha baada yake likafuatilia neno jengine liloanzia na hamza basi inajuzu katika hali ya wasl kuivuta herufi ya madda imma kwa harakah nne, tano au sita na pia inajuzu kuifupisha ikawa harakah mbili. Amma katika hali ya kusimama kwa Mfano tukisimama kwenye ( اِنَّا ) bila ya kuunganisha ( أَعْطَيْنَاكَ ) basi hapo itawajibika kuvutwa harakah mbili tu kwa sababu itakuwa ni madda ya asili katika hali hii.
Mfano katika hali ya wasl: قَالُوا إِنَّا ، َوَفِي أنْفُسِكُم ، هؤُلاَء
Inshaallah tutaendelea kwenye darsa zijazo
|
|||
| 1 2 | |||
|
|
|||