| BACK TO LIST | ||
|
باب المدّ Mlango wa madda
Herufi za madda ni tatu nazo ni: ا ، و ، ي
Zimekusanywa kwenye neno hili: نُوحِيهَا
Madda ni kuirefusha sauti ya herufi ya madda (kama tulivyokwishazitaja hapo juu). Herufi ya madda huzidi kuvutwa inapokutana mbele yake na hamza au sukun.
Madda zimegawika katika makundi mawili makuu 1- Madda ya asili na الْمَدُّ الاَصْلِيّ 2- Madda iliyozidi الْمَدُّ الْفَرْعِيُّ
Madda ya asili الْمَدُّ الاَصْلِيُّ au اَلْمَدُّ الطَّبِيعِيُّ
Madda hii inakuwa kwenye ile herufi yenyewe ya madda ambayo kama haijavutwa herufi hiyo ya madda basi inakuwa madda haijapatikana bado na huenda isilete maana ya hilo neno. Madda ya asili haitanguliwi baada yake na hamza wala sukun. Mfano: قَالَ، = qaAAla, يَقُوْلُ = yaquUUlu, قِيْلَ = qiIIla
Makadirio ya kuivuta kwake ni harakah mbili kama tulivyoona katika mfano, ikiwa katika hali ya kupita (wasl) au kusimama (waqf), hakuzidishwi kuvutwa kwake wala hakupunguzwi. Na ndio maana ikaitwa madda ya asili.
2-Madda iliyozidi (ya ziyada) الْمَدُّ الْفَرْعِيُّ
Hii ni madda inayovutwa zaidi kuliko ile madda ya asili kwa sababu ya kutokea (a) hamza, au (b) sukun baada ya herufi ya madda.
|
||
| 1 2 | ||
|
|
||