BACK TO LIST

 

       IDH_HAR   IDGHAM   IQLAB   IKHFAA' 

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Hukmu za nūni iliyokuwa săkinah نْ   na tanween  ً ٍ  ٌٌ   

 

Nuni iliyokuwa săkinah na tanween ina hali nne nazo ni:-

 

IDH-HAR

IDGHAM

IQLAB

IKHFAA

 

IDH-HAR

 

Idh-har katika somo hili maana yake ni kuidhihirisha kimatamshi nuni yenye sukun (nuni sakna) au tanween kwa kuitoa kwenye matokeo yake khasa kama hivi “ nnn” bila ya kuitia ghunnah (Ghunnah ni sauti itokayo puani).

 

Nuni hiyo au tanween itadhihirishwa ikiwa mbele yake itatokea herufi kati ya herufi 6 za Idh-har (zenye fat-ha kasra au dhamma) nazo ni :-

Hamza 

  ء
Haa   هـ
A’yn   ع
Haa   ح
Ghayn    غ
  Khaa   خ

                                                                              

 

Kwa urahisi wa kuzikumbuka herufi hizi, ziko  mwanzo wa kila neno kwenye beti hii ya ushairi:-

أََخِي هَاكَ عِلْمًا حَا زَهُ غَيرُ خَاسِر  

 

Sasa Tuangalie mifano ili tupate kujuwa namna gani tunaweza kuitambua hii hukmu ya Idh-har.

 

Kwanza tufahamu kwamba nuni yenye sukun (sakna) hutokezea kwenye neno moja au maneno mawili tofauti kama tutakavyoona kwenye mithali:-

 

مَنْ  أ ٰ مَنَ

 

  Kwa hiyo hapa tutadhihirisha nuni săkinah kwa sababu mbele yake ipo alif nayo ni herufi ya Idh-har. Tunasoma bila ya kutia ghunnah

 

MAN AAMANA

 

NEXT 

  Site Meter