| BACK TO LIST | |||||||||||||||||||||||||
| IDH-HAR IDGHAM IQLAB IKHFAA' | |||||||||||||||||||||||||
|
Idgham itiwayo ghunnah ا دغا م بغنة
Ikitokezea nūni iliyokuwa săkinah نْ au tanween ً ٍ ٌ na mbele yake ikawepo herufi moja kati ya herufi hizi يَنْمُو yaani ي ن م و hubadilishwa sauti ya نْ au tanween mpaka ikawa imefanana na sauti ya herufi ya mbele yake ikisha ikatoka sauti iliyotiwa shaddah na yenye ghunnah.
Kabla ya kudaghamisha:-
Baada ya kudaghamisha:-
Kudaghamishwa kwa namna hii kunapatikana kwenye maneno mawili; moja liwe limemalizikia na نْ au ً ٍ ٌ na neno linalofuata liwe limeanzia na herufi za يَنْمُو
Mifano ya Idghăm itiwayo ghunnah ا دغا م بغنة Kuangalia miafano, bonyeza hapa Endapo inatokea “ نْ” na mbele yake ikafuata herufi moja kati ya herufi za يَنْمُو kwenye neno moja, basi hukmu ya idghăm huondoka na hairuhusiwi kudaghamisha kwenye maneno halo bali tunatamka neno hilo kama lilivyo. Mfano:
Na katika Qur-ăn nzima kuna maneno haya tu mane yenye sifa ya idghăm lakini hayadaghamishwi kwa sababu idghăm hiyo iko kwenye neno moja.
Kwa hiyo tukiyaona maneno haya katika Qur-ăn tujuwe kuwa hukmu yake ni kuyatamka kama yalivyo. والله اعلم |
|||||||||||||||||||||||||
| 1 2 3 | |||||||||||||||||||||||||
|
|