BACK TO LIST
       IDH-HAR   IDGHAM   IQLAB   IKHFAA' 

بسم الله الرحمن الرحيم

  

(B) AL IDGHĂM الادغا م                                                

      

Hali ya pili ya nūni iliyokuwa săkinah  na tanween   inaitwa idghăm.

 

Idghăm maana yake ni kuzichanganya herufi mbili kuwa ni herufi moja yenye shaddah  ّ  , kwahiyo hapa tutatumuia neno kudaghamisha’ ili kufupisha maneno.

 

Idghăm ina herufi sita (6) nazo ni:

YAA   ي
RAA   ر
MIYM   م
LAAM   ل
WAAW   و
NUUN   ن

                

kwa urahisi wa kuzikumbuka herufi hizi zimewekwa kwenye neno hili:

 

YARMALUUNA   يَرْمَلُونَ

  

 

Herufi mbili (2) kati ya hizi ni za kudaghamisha bila ya ghunnah na herufi nne (4) zilizobaki ni  za kudaghamisha pamoja na kutia ghunnah.

 

 

 

Idghăm imegawika sehemu mbili:-

 

 1.      Idghăm isiyotiwa ghunnah na                        ١-  ا دغا م بلاغنة

2.     Idghăm yenye kutiwa ghunnah                         ٢-   ا دغا م بغنة

       

1.    Idghăm isiyotiwa ghunnah herufi zake ni mbili (2) tu nazo ni:                                                                                   

RAA  

ر

LAAM    ل

                 

Kwa urahisi wa kuzikumba herufi hizi zinapatikana kwenye neno lifuatalo: 

    

RALLA   رَ لَّ

 

2.   Idghăm yenye kutiwa ghunnah herufi zake ni nne (4) nazo ni:

                     

YAA   ي
NUUN   ن
MIYM   م
WAAW   و

             

Kwa urahisi wa kuzikumba herufi hizi zinapatikana kwenye neno lifuatalo:  

      

YANMUU  

يَنْمُو

1 2 3
  Site Meter